×

Nchi Zenye Utajiri Mkubwa Zaidi Afrika

BENKI ya Dunia imezitaja nchi za Afrika zilizo na utajiri mkubwa zaidi  wa asili licha ya kuwa miongoi mwake ni maskini na zikiwa katika mazingira mbalimbali magumu kwa sasa ambapo inategemewa mwaka 2025 pato la taifa (GDP) kwa kila mtu (kwa kipato cha kati) katika nchi hizo litafika Dola 1,000.  (Sh. mil. 2.2).

Hivi sasa Afrika ina watu bilioni 1.3 waliomo katika nchi 54 na pato lao la jumla la taifa likifikia Dola bil. 2.2.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Ina utajiri mkubwa hususan wa madini, utajiri ambao hautumiki ipasavyo kwa watu wake ambao ni zaidi ya milioni 84, hivyo kuifanya iwe  moja ya nchi zenye watu maskini zaidi za Afrika na duniani ambapo pato lake kwa taifa, yaani GDP ni Dola 478.23.

Uganda

Uganda ni moja ya nchi tajiri zaidi Afrika kwa maliasili, ikiwa na pato la Dola bil. 25.53  na watu mil. 44.27, lakini ni moja ya nchi 10 maskini zaidi duniani.

Ethiopia

Ethiopia ni nchi ya pili kwa idadi ya watu Afrika – mil. 107.53.    GDP yake ni Dola bil. 80.87 na utajiri mkubwa wa madini na mazao, lakini ni miongoni mwa nchi ambazo watu wake maskini Afrika na duniani.

Niger

Niger ina GDP ya Dola 444 na watu  mil. 22.3 ambapo pamoja na utajiri mkubwa wa asili watu wake ni miongoni mwa maskini duniani.

Nigeria

Nigeria ni nchi tajiri na idadi kubwa zaidi ya watu Afrika ambayo ni mil 195.8,  GDP ya Dola bil. 376.28  lakini  kiuwiano, watu wake wengi bado ni maskini.

Zimbabwe

Uchumi wa Zimbabwe ulioporomoka tangu miaka ya mwanzo ya  2000, umeifanya kuwa na GDP ya Dola bil. 17.1 kwa watu mil. 16.9.

Zambia

Maliasili za Zambia ni nyingi lakini hazitumiki ipasavyo kwa watu wake mil. 17.6 na GDP yake ya Dola bil. 23.1, hivyo umaskini kwa watu wake unaendelea licha ya kukua kwa uchumi wake.

Madagascar

Madagascar inayotegemea utajiri mkubwa wa utalii bado haijaondoa,  kwa kiwango cha kuonekana,  umaskini kwa watu wake mil. 26.2 na GDP ya Dola bil. 10.3.

South Sudan

South Sudan moja ya nchi maskini zaidi Afrika licha ya maliasili kibao kwa watu mil. 12.9 na GDP ya Dola bil. 275.  Asilimia 24 tu ya wananchi wake wamesoma; maeneo mengi zaidi hayana umeme wala maji salama ya kunywa.

Senegal

Senegal ina utajiri mkubwa wa kilimo, utalii, mazao na kadhalika.  Ina watu mil. 16.2 na GDP ya Dola bil. 16.1.

Kenya

Kenya ina watu mil. 50.95 na GDP ya Dola mil. 79.51 ikishika nafasi ya tisa kwa utajiri Afrika, lakini hali ya wananchi wake wengi wako katika umaskini.

Tunisia

Tunisia ina watu mil. 11.6, GDP ya Dola bil. 40.2 lakini bado haijakidhi kuondoa umaskini kwa watu wake.

Ivory Coast

Ivory Coast ina watu mil. 24.9 GDP ya Dola bil. 53, lakini bado haijautumia vyema utajiri huo kwa wananchi wake.

Algeria

Algeria yenye akiba kubwa ya gesi na mafuta ina GDP ya Dola bil. 173 ikiwa miongoni mwa nchi tano tajiri zaidi Afrika.

Afrika Kusini

Ina GDP ya Dola bil. 349.29 na watu mil. 57.3 na utajiri wa aina nyingi, ikiwa miongoni mwa nchi sita tajiri zaidi Afrika.

Misri

Misri nchi yenye historia inayoanzia karne ya sita Kabla ya Yesu, ina utajiri mkubwa wa kila aina wa asili, ikishika nafasi ya tatu kwa uchumi wenye nguvu zaidi Afrika.  Ina GDP ya Dola bil. 237.03.

Angola

Angola ina utajiri mkubwa wa mafuta na mazao.  GDP yake ni Dola bil. 124.209, ikishika nafasi ya tano kwa utajiri barani Afrika.

Morocco

Morroco inashika nafasi ya sita kwa utajiri Afrika.  Ina watu mil. 36.1 na GDP ya Dola bil. 109.82.

Sudan

Sudan ni nchi ya tisa kwa idadi ya watu ambao ni mil. 41.51.  Kwa utajiri inashika nafasi ya tisa na ina GDP ya Dola bi. 58.23.

Tanzania

Tanzania ina GDP ya Dola bil. 51.72 na inashika nafasi ya kumi katika nguvu za uchumi barani Afrika.

Ghana

Ghana ina GDP ya Dola bil. 47.03, ikishika nafasi ya 11 kwa utajiri Afrika ambapo ina watu mil. 29.46.