WAREMBO WATAKAOTIKISA MISS TANZANIA 2018 NI SHIDA
WAREMBO ambao wanashiriki katika Shindano la Miss Tanzania 2018, leo Alhamisi, Agosti 30, wametembelea makao makuu ya ofisi za Makampuni ya Global Group na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na makampuni hayo ikiwemo uzalishaji wa magazeti.
Walimbwende hao walifika katika Ofisi za Global Group ambazo ndani yake kuna Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Kiswahili yanayoongoza kwa habari za michezo nchini ya Championi na Spoti Xtra.
Mbali na kujionea uzalishaji wa magazeti pendwa ya Ijumaa, Risasi, Uwazi, Amani na Ijumaa Wikienda, pia walipata nafasi ya kutembelea studio za Global TV Online na kufanya mahojiano ambayo baadaye utayatazama kupitia YouTube channel ya Global TV.
Comments are closed.