
Makontena yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, yamepigwa mnada tena leo Jumamosi, Septemba 1, 2018 na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika bandari ya Dar es Salaam baada ya kushindwa kuyalipia kodi ya Tsh bilioni 1.2.

“Mpaka sasa tayari tumefanya mnada wa makontena yote 20 lakini hayajapata mteja ingawa tumefanikiwa kuuza bidhaa 10 zilizokuwemo kwenye makontena hayo. Hivyo mnada wa makontena utaendelea tena Jumamosi ijayo.” amesema Scolastika Kevala, Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya YONO AUCTION MART.