×

PIKIPIKI YA 11 TUSUA MAISHA NA GLOBAL YAENDA TUKUYU

Ndagha fijho! Hivyo ndivyo alivyosema mshindi wa pikipiki katika droo ya 11 ya Shindano la Tusua Maisha na Global, Bolen Kilimba akimaanisha ‘asante sana’ baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa zawadi hiyo chini ya udhamini mnono wa Sokabet.

 

Kilimba, mkazi wa Tukuyu, Mbeya ametangazwa kuwa mshindi Jumanne ya Septemba 4, 2018 katika droo iliyorushwa mubashara na kituo cha runinga cha Global TV Online na kujishindia pikipiki hiyo mpya kabisa.

 

Wengine waliong’ara katika droo hiyo ni Silvanus Nyombe wa Mwana aliyejishindia dinner set na Eliuter Ndunguru wa Manyoni, Singida, aliyejishindia jezi. Baada ya kufanyika kwa droo hiyo, sasa imesalia droo moja na ya mwisho, itakayochezeshwa Jumanne ijayo na kuhitimisha shindano hili lililobadilisha maisha ya wasomaji wengi.

 

Wakati huohuo, washindi wa droo ya tisa na kumi, wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao wakati wowote kuanzia sasa. Wanaotarajiwa kukabidhiwa zawadi zao, ni Ramadhan Simba, mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam aliyejishindia pikipiki, Anna Mbise wa Arusha aliyejishindia dinner set na Hussein Mtipa wa Ifakara, Morogoro aliyejishindia jezi.

Wengine ni Ramadhan Mohamed wa Zanzibar aliyejishindia pikipiki, Geofrey John mkazi wa Chanika aliyejishindia dinner set na Justice Rugambwa mkazi wa Gongolamboto aliyejishindia zawadi ya jezi.

 

Ili kushiriki katika dakika za lala salama, nunua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers kati ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra. Ukishanunua, funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki.

Itume namba maalumu inayoonekana juu ya kuponi kwa njia ya meseji kwenda namba 0719386533. Hakikisha unahifadhi kuponi au gazeti lako kwani linahitajika wakati wa kuchukulia zawadi.

PIKIPIKI YA 11 TUSUA MAISHA NA GLOBAL YAENDA TUKUYU