The House of Favourite Newspapers

NDOA KUMBADILI DINI SISTER FEY

Faidha Omary ‘Sister Fey’

NI kama igizo! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na kwamba licha ya mpenzi wake, Elias John ‘Holly Star’ kuwa mdogo kiumri ‘kiben’teni’, msanii wa filamu na muziki Bongo, Faidha Omary ‘Sister Fey’ amefunguka kuwa yupo kwenye mpango wa kubadili dini na kuwa Mkristo ili waweze kufunga ndoa.  

 

Akizungumza na Za Motomoto News, Fey alisema kwa sasa wako kwenye mipango ya kuingia kwenye ndoa harakaharaka kwa kuwa ni mjamzito hivyo yupo radhi kubadili dini kwa sababu amependa kweli.

 

“Tuko kwenye mipango ya ndoa na ndani ya miezi miwili hii tutafunga ndoa, niko tayari kubadili dini, tunasubiri tu uamuzi kutoka kwa babamkwe kwamba tutafunga ndoa ya bomani au kanisani.

 

“Sioni shida kubadili dini au kuolewa na kijana huyo, kisa namzidi umri kwa sababu hakuna asichokijua kwenye dunia hii, nampenda na siwezi kumuacha ndiyo maana niko tayari kubadili dini nimfuate kwenye ukristo kama mzazi wake ataamua hivyo,” alisema Fey.

Stori: Gladness Mallya, Dar

Comments are closed.