KAMPUNI ya Mega Beverages Company Limited, yenye makao yake makuu mjini Arusha, imezindua chupa mpya za kinywaji chake cha K-Vant mkoani Arusha, katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Mount Meru.
Uzinduzi wa Arusha unafuatia uzinduzi mkubwa uliofanyika jijini Dar es Salaam mapema wiki iliyopita.
Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni hiyo, Bw. Marco Maduhu alisema “Tunayo furaha kubwa kuwashirikisha wateja wetu katika uzinduzi huu wa chupa yetu mpya hapa mkoani Arusha ambapo tunapaita nyumbani kwetu. Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa washirika wetu katika biashara, wadau na wateja wetu kwa kuendelea kutuunga mkono”, alisema.
Mbali na uzinduzi uliofanyika Dar es Salaam na Arusha, alisema uzinduzi mwingine wa chupa mpya utafanyika mkoani Mwanza, ingawa usambazaji wa bidhaa za K-Vant ndani ya chupa mpya tayari umeanza kufanyika nchini kote.
Maduhu alieleza pia kuwa Mega Beverages Company Limited, itaanza kufanya kampeni kubwa ya kuendeleza masoko ya bidhaa zake, ambayo italenga masoko ya ndani na masoko katika nchi za Afrika Mashariki, kuhakikisha zinapatikana kwa urahisi mahali pote.
Kampeni hiyo inatarajiwa kufanikisha ongezeko la uzalishaji, hali ambayo itawezesha kampuni kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuchangia kukuza uchumi wa nchi.
Comments are closed.