×

Video: MASHINJI “Nani Aliwafundisha Kuweka Mimba, Mnataka Wafe?”

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezungumzia kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa akiwa ziarani mkoani Simiyu akiwataka wananchi wazae tu idadi ya watoto wanaotaka kwa sababu serikali ina uwezo wa kuwasomesha watoto hao bure na tayari inapeleka pesa hizo mashuleni kila mwezi.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vincet Mashinji amesema Serikali ina wajibu wa kuhakikisha inatoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wake kwa ajili ya kuboresha afya na kupata vizazi vitakavyolisaidia Taifa.

 

“Tunasema tuzae bila kikomo, kuzaa ni jambo jema, hakuna anayepinga kuzaana lakini tuzae kwa mpango, mpangop wa taifa umeelekeza zitengwe fedha kwa ajili ya kutoa elimu ya uzazi wa mpango ili tupate taifa la wazalishaji kwa maendeleo ya taifa hili.

 

“Kila ongezeko la watoto linasababisha kuongezeka kwa msongamano darasani, tamko la kuzaana bila kikomo limetolewa Simiyu mkoa ambao watu wake wanazaliana kuliko eneo lolote nchini, ni mkoa uliyo na wananchi wengi wasiojua kusoma na kuandika.

 

“Hivi ni nani kati yenu alikwenda kufundishwa jinsi ya kuweka mimba kwa mwanamke au kupokea mimba kutoka kwa mwanamme? Tusipowafundisha hawa watoto tutegemee ongezeko la mimba za utotoni, Ni jukumu letu kuendelea kuwafundisha kuhusu uzazi wa mpango kwa ajili ya maeneleo ya taifa letu.

 

“Kwa mwanamme ni rahisi sana kusema abebe mimba tu, lakini mwanamke anafahamu kichefuchefu anachokipata, madhara wakati wa kujifungua, wanaume wote tunaowajali wanawake tuungane kuhakikisha tunaimarisha uzazi wa mpango na kupeleka wake zetu kliniki.

 

“Nyie mnataka wake zetu wawe wanakufa tu hospitalini kwa sababu mnaweza kuoa wake wengine? Hii haikubaliki. Msimamo wa Chadema ni kwamba, watoto wote katika Taifa hili wenye umri wa kwenda shule wapelekwe bila kujali jinsia wala jinsi yake. Tunaambiwa hawa mabinti waliopewa mimba wasirudi shule kusoma, kama unazuia uzazi wa mpango unadhani wataachaje kupata mimba?” amesema Mashinji.

VIDEO: MSIKIE MASHINJI AKIFUNGUKA