The House of Favourite Newspapers

Mzungu Wa Simba Anakula Kwa Mama Ntilie

Patrick Aussems

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa licha ya kutokujua kupika lakini anakula chakula chochote atakachopewa kwa kuwa hachagui cha kula huku akisisitiza kuwa ameshaanza kula vya uswahilini kwa mama ntilie.

 

Aussems raia wa Ubelgiji amepangiwa kwenye Hoteli ya Sea Scape iliyopo Mbezi Beach ambayo gharama yake ni kubwa ikiwa ni bada ya kocha huyo kukataa kuishi kwenye nyumbani za kupangiwa.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Aussem alisema kuwa katika maisha yake hajawahi kuchagua chakula katika sehemu zote alizofundisha hula chochote kinachokuwa kimeandaliwa.

 

“Unajua sijui kabisa kupika chochote na ndiyo sababu ya kukataa kukaa nyumba ya kupanga kwa kuwa mara zote sipendi kuletewa wapishi maalum hilo sipendi kabisa kwa kuwa mimi sichagui chakula.

 

“Nimefanya kazi China, Nepal, Sudan, Cameroon, Benin na hata Congo Brazza Ville huko kote nilikuwa nakula vyakula vyote ambavyo wenyeji wangu wana kula hata hapa nafanya hivyo kwa sababu siku tuliyocheza na FC Loepards nilienda kula sehemu ya chini ‘mama ntilie’ chakula cha kawaida kabisa japo sijui wanaitaje ila kama ladha ikinishinda huwa nakiacha,” alisema Aussems

 

Comments are closed.