The House of Favourite Newspapers

SIMANZI MV NYERERE: Apoteza Watoto Wawili, Ndugu Watatu – VIDEO

WAKATI Simanzi na majonzi vimetawala kwa Taifa zima kutokana na ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kiliyozama jana katika Ziwa Victoria, ndugu Yustus Mziray Majula Mlima ambaye ni mzaliwa wa Kata ya  Jang’ombe, Tarafa ya Ukara amedai kupoteza ndugu zake watano kutokana na ajali hiyo.

 

Ystus amesema amepoteza dada yake, aitwaye Ester Mkome Mrembwe wa Nyamanga, shemeji yake ambaye ni mke wa mdogo wake, Matatizo Mabiba, mdogo wake, Lameck Mabangida na watoto wake wawili.

 

Mpaka sasa miili zaidi ya 100 imepatikana katika ajali hiyo inayokadiriwa kulikuwa na abiria 400 huku majeruhi 37 wakiokolewa na kupelekwa Kituo cha Afya Bwasha, Ukara kupatiwa matibabu kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

VIDEO: MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA

Comments are closed.