The House of Favourite Newspapers

BREAKING: MHANDISI WA MV NYERERE AOKOLEWA AKIWA HAI – VIDEO

#BreakingNews: Mhandisi wa Kivuko cha MV Nyerere kilichopata ajali ya kuzama katika Ziwa Victoria juzi, Alphonce Augustino Cherehani ameokolewa muda mfupi uliopita akiwa hai.

 

Charahani ameokolewa leo Jumamosi Septemba 22, 2018 majira ya saa 4:45 asubuhi ikiwa ni takribani saa 48 tangu kuzama kwa kivuko hicho na kukimbizwa Kituo cha Afya cha Busya kilichopo katika Kisiwa cha Ukara.

 

Mmoja wa wazamiaji ambao wanafanya zoezi la kuokoa amesema tangu juzi Septemba 20, 2018 kilipozama kivuko hicho kila walipokuwa wakigonga walisikia mtu mwingine akigonga kwa ndani.

 

Baadhi ya wazamiaji wanaoopoa miili wamesema Charahani alikuwa amejipaka oili mwili mzima ili maji yasiweze kupita kwenye vinyweleo vyake na kuingia kwenye mfumo wa mzunguko wa damu.

 

Aidha, amesema alianza kugonga jana usiku akiomba msaada na leo asubuhi ndiyo sauti yake ilisikika akaokolewa.

TAZAMAINJINIA CHEREHANI ALIVYOOKOLEWA

Comments are closed.