×

Chadema Wanazindua Sera Toleo la Mwaka 2018, Dar

Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dr.Vincent Mashinji, akiongea jambo katika uzinduzi wa Sera toleo la mwaka 2018 ya chama hicho katika hoteli  ya Ledger Plaza , Bahari Beach jijini Dar.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, leo Jumanne, Septemba 24, 2018, wamezindua upya Sera zake toleo la 2018 katika hoteli  ya Ledger Plaza , Bahari Beach jijini Dar.

Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiwa ndani ya ukumbi wa Bahari Beach jijini Dar.

Katika uzinduzi huo,  Chadema wameweka hadharani misimamo ya kisera kwenye maeneo mbalimbali ya uchumi, afya, elimu na sayansi, miundombinu, maji, mfumo wa Utawala, Katiba na haki za binadamu, Masuala ya Muungano, Mambo ya Nje na Uhamiaji, Siasa za ndani, Usimamizi wa Ardhi na Kilimo pamoja na Mazingira.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akiendelea kusikiliza wajumbe mbalimbali (hawapo pichani).

Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dr.Vincent Mashinji, amesema wakati wa uzinduzi wa Sera hizo mpya kuwa wametumia mwaka mmoja kufanya mabadiliko hayo ili kuleta maboresho ya Sera baada ya kuangalia Sera za nchi zilizofanikiwa ulimwenguni.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiongea jambo wakati wa uzinduzi.
Wabunge wa Chadema wakiendelea kumsikiliza Freeman Mbowe kutoka kushoto ni Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.
Wanachama wa Chadema na wadau mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye (wa pili kutoka kushoto) akiwa amekaa  na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari (wa pili kutoka kulia), aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu (kulia) na kushoto ni  Naibu katibu mkuu Chadema Zanzibar,Salum Mwalimu.

   PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL