×

RC HAPI AMSIMAMISHA KAZI OFISA WA USTAWI WA JAMII – VIDEO

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi,  amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kumsimamisha kazi Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa,  Martin Sitta, kutokana na kutoa taarifa kwa watu wenye ulemavu wa kutosikia kuwa fedha zimetumika katika ziara ya mkuu huyo wa mkoa.

Hapi amesema hayo leo wakati alipotembelea Shule ya Viziwi na kusikiliza malalamiko ya baadhi ya watu wenye ulemavu huo ambao wamemweleza kuwa wameshindwa kwenda kwenye mafunzo Dodoma kutokana kuambiwa na ofisa huyo kuwa fedha zimeenda kwenye ziara aliyofanya yeye (Hapi).

 

Akitoa maelezo,  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania, Shaibu Juma,  amesema walipeleka barua kwa katibu tawala wa mkoa na aliwaamuru kuipeleka ofisi za Manispaa ili kushughulikiwa ambapo waliandikiwa barua kuwa fedha hizo zimetumika kwenye ziara hiyo.

 

Baada ya Hapi kuisoma barua hiyo,  Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Hamid Njovu, akalazimika kulitolea ufafanuzi suala hilo mbele ya Hapi.

Baada ya mkurugenzi huyo kutoa ufafanuzi, Hapi alimwagiza Kaimu Katibu Tawala, Fikiri Kisimba, kuandika barua  wizarani kutomtaka mkoani mwake ofisa huyo,  na nyingine kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,  Juma Bwire,  ili amtafute ofisa huyo na kumkamata.

Kwa taarifa na Albert Eliud

Yaani Anatumikia Bwana Mwingine, RPC Mkamateni, Afukuzwe Kabisa