
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimepata pigo jingine baada ya Mbunge waake wa Serengeti mkoa wa Mara, Marwa Chacha Ryoba kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge, kujivua uanachama na kuhamia CCM kwa madai ya kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Ryoba aliyefanya maamuzi hayo usiku wa kuamkia leo, Septemba 28, amesema wakati akigombea ubunge aliahidi kuwaletea maendeleo wananchi wake lakini dhamira yake haijafanikiwa kutoka na vikwazo anavyokumbana navyo ndani ya Chadema.
Chacha amewataka wakazi wa Serengeti kumchagua mtu atakayeweza kushirikiana nao pamoja ili kuleta maendeleo kupitia CCM.