
MWENYEKITI wa kamati ya Maafa ya Kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Isaac Kamwelwe leo amepokea michango kutoka mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na kusema fedha zote zlizobaki zimeelekezwa na Rais Magufuli zijenge wodi tatu (ya wanawake, wanaume na ya watoto na fenicha zake ndani) katika Kituo cha Afya Bwisya wilayani humo.
Kamwelwe ametangaza kiasi cha fedha alichpokea kutoka sehemu tofauti huku akitoa shukrani zake za dhati kwa wale ambao wameguswa na kuchangia fedha na kwa wale ambao wameguswa na tukio hilo na kusema Rais ameagiza pesa hizo zitumike kwa matuzmizi yaliyopangwa na si vinginevyo.
Ili kufanikisha zoezi la ujenzi huo na gharama ndogo, Kamwelwe amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kununua materials za ujenzi, matofari, mabati na vyote vinavyotakiwa kisha kutafuta fundi wa ujenzi watakaofanya shughuli hiyo badala ya kutangaza tenda ambayo amedai inaweza kuchukua gharama kubwa.
Aidha, Serikali imehitimisha zoezi la uokoaji na uopoaji wa watu na miili uliotokana na ajali ya kupinduka kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea Septemba 20 na kuua watu 230.