Mmoja wa wasomaji wa Gazeti la Spoti Xtra (kushoto) akijaza kuponi ya shindano la kujishindia jezi orijino au zawadi nyingine nyingi.




MAPEMA leo katika jiji la Dar es Salaam, eneo la Uwanja wa Taifa, mashabiki wa klabu za Simba na Yanga wamelichangamkia gazeti la Spoti Xtra linalotoka kila Jumaili kwa bei ya Sh.500/= na kujaza kuponi za shindano la kujipatia zawadi za jezi orijino na zawadi nyingine mbalimbali.
Kikosi kazi cha promosheni ya Spoti Xtra leo kiliendelea kulinadi gazeti hilo kwa wasomaji ambapo lilipita sehemu mbalimbali na kisha kutua Uwanja wa Taifa ambapo kuna mpambano wa watani wa jadi, Simba na Yanga.
Picha: Richard Bukos.