The House of Favourite Newspapers

BENKI YA DTB YAKABIDHI VYOO KWA SHULE YA MSINGI UKONGA

Mkuu wa kitengo cha Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester Bahati akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vyoo kwa shule ya Msingi ya Ukonga vilivyojengwa kwa thamani ya shilingi milioni 48 za kitanzania. Msaada huo ni sehemu ya wajibu wa kijamii wa benki hiyo wenye lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia sambamba na viwango vya elimu kwa wanafunzi nchini. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Ukonga wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Jumaa Mwipopo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ukonga wakati wa hafla ya kupokea vyoo vilivyojengwa na Benki ya Diamond Trust bank (DTB) kwa ajili ya shule hiyo iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam. Msaada huo ni sehemu ya wajibu wa kijamii wa benki hiyo wenye lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia sambamba na viwango vya elimu kwa wanafunzi nchini. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Ukonga wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Jumaa Mwipopo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ukonga wakati wa hafla ya kupokea vyoo vilivyojengwa na Benki ya Diamond Trust bank (DTB) kwa kiasi cha shilingi milioni 48 kwa ajili ya shule hiyo iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam. Msaada huo ni sehemu ya wajibu wa kijamii wa benki hiyo wenye lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia sambamba na viwango vya elimu kwa wanafunzi nchini. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Benki ya DTB, Tawi la CBD, Bw. Jonas Mbuya.
Meneja wa Benki ya DTB, Tawi la CBD, Bw. Jonas Mbuya akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ukonga (hawapo pichani) katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam ambapo benki hiyo ilikabidhi msaada wa vyoo kwa shule hiyo vilivyogharimu kiasi cha shilingi milioni 48. Msaada huo ni sehemu ya wajibu wa kijamii wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB) wenye lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia sambamba na viwango vya elimu kwa wanafunzi nchini.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Ukonga, Violeth Luanda akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vyoo vilivyojengwa kwa hisani ya benki ya Diamond Trust Bank (DTB) kwa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 48, iliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Msaada huo ni sehemu ya wajibu wa kijamii wa benki hiyo wenye lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia sambamba na viwango vya elimu kwa wanafunzi nchini.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Ukonga, Violeth Luanda akisalimiana na Meneja wa Benki ya DTB, Tawi la CBD, Bw. Jonas Mbuya mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam, wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vyoo vilivyojengwa na benki hiyo kwa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 48. Msaada huo ni sehemu ya wajibu wa kijamii wa benki hiyo wenye lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia sambamba na viwango vya elimu kwa wanafunzi nchini.
Diwani wa Kata ya Ukonga wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Jumaa Mwipopo (katikati) akikata utepe kufungua rasmi jengo la vyoo lililojengwa kwa hisani ya benki ya Diamond Trust Bank (DTB) kwa ajili ya Shule ya msingi ya Ukonga kwa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 48, katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Msaada huo ni sehemu ya wajibu wa kijamii wa benki hiyo wenye lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia sambamba na viwango vya elimu kwa wanafunzi nchini. Pamoja nae ni Meneja wa Benki ya DTB, Tawi la CBD, Bw. Jonas Mbuya (kushoto) na Meneja wa tawi la barabara ya Nyerere, Zainab Rashid (kulia).

 

Benki ya Diamond Trust Bank (DTB) imekabidhi  rasmi jengo la vyoo  Shule ya msingi ya Ukonga lililojengwa kwa hisani ya benki hiyo kwa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 48.

Comments are closed.