×

Kamwele Awatimua Wachina Wawili kwa Kuwapiga Watanzania

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Isack Kamwelwe, amewafukuza na kuwaamuru waondoke nchini mara moja raia wawili wa China kwa makosa la kuwapiga na kuwanyanyasa Watanzania walioajiriwa kufanya kazi katika Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Chunya – Makongorosi mkoani Mbeya.

 

Kamwelwe ametoa amri hiyo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza ya kutembelea mradi wa ujenzi wa barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami, lakini akiwa njiani akasimamishwa na wananchi wa Kijiji cha Matundasi wilayani Chunya ambao wamemueleza kuwa wasimamizi wa mradi huo ambao ni Wachina (wanafanya kazi kwenye Kampuni ya China Railway Co. Ltd) wanawanyanyasa kwa kuwapiga, kuwatishia kuwaua kwa silaha za moto, kuwakata mishahar na kuwafukuza kazi bila sababu za msingi.

 

 

Baada ya kupokea malalamiko hayo, Kamwelwe akahoji utendaji kazi wa kampuni hiyo katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo, na ndipo mwakilishi wa Kampuni ya Smec Company Ltd inayosimamia mradi huo kwa niaba ya serikali, Gosbert Luburi, akaeleza kuwa mradi huo uko nyuma ya ratiba ikilinganishwa na makubaliano ya mkataba wa ujenzi huo.

 

 

Eng. Kamwelwe amesema kuwa barabara hiyo inajengwa kwa kodi za Watanzania kwa asilimia 100, na kwa mantiki hiyo Watanzania ndiyo waliowaajiri Wachina hao kupitia kodi zao, hivyo serikali haiwezi kuvumilia unyanyasaji wa aina hiyo ambao ameufananisha na ukoloni, ndipo akatoa uamuzi wa kuwatimua mara moja Wachina hao waliodaiwa na wananchi kuwa ndiyo vinara wa unyanyasaji dhidi yao.

RC AMEMUITA RPC KAMPA MAAGIZO “KAMATA WEKA NDANI”