The House of Favourite Newspapers

Mbunge wa Rorya Aagiza Baba Yake Akamatwe

MARA: Mbunge wa Rorya (CCM), Lameck Airo,  ameliagiza jeshi la polisi kumkamata baba yake mdogo baada ya kutajwa katika mkutano wa hadhara akituhumiwa kuhusika na wizi wa mifugo.

Wanakijiji wa Koryo, Wilaya ya Rorya mkoani Mara, wamemlalamikia mzee huyo kwa kuiba ng’ombe na kuwauza katika minada ya ndani na nje ya wilaya hiyo.

 

Mkuu wa polisi wa wilaya hiyo, Ramadhan Sarige, amewapongeza wananchi hao kwa ushirikiano walioanza kuutoa kwa vyombo vya dola katika kukabiliana na vitendo vya wizi wa mifugo.

 

Mkutano umefanywa ikiwa ni sehemu ya kampeni inayofanywa na vyombo vya dola kupambana na wimbi kubwa la wizi wa mifugo lililoibuka siku za karibuni wilayani humo

Chanzo; ITV.

Comments are closed.