×

AJIBU: MBWANA SAMATTA AMENIACHIA UJUMBE MZITO

KIKOSI cha Yanga, kesho Jumamosi kinashuka uwanjani kupambana na Alliance FC katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu amesema endapo atapata nafasi ya kuitumikia timu yake hiyo katika mchezo huo basi amepanga kuingia uwanjani huku akili yake ikiwa imetawaliwa na ujumbe mzito alioachiwa na mshambuliaji wa kimataifa wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta.

 

Ujumbe huo ambao Ajibu ameachiwa na Samatta ambaye hivi karibuni alikuwa hapa nchini kwa ajili ya majukumu ya timu ya taifa, Taifa Stars ni kuhakikisha anajituma vilivyo ili aweze kuisaidia timu yake ya Yanga kufanya vizuri msimu huu.

 

Ajibu ameliambia Championi Ijumaa kuwa, ujumbe huo ambao Samatta amemwachia siyo kwamba walikaa pamoja na kuzungumza bali ni ule wa vitendo ambao alibahatika kuuona kutoka kwa mshambuliaji huyo wakati alipokuwa uwanjani akitumikia Taifa Stars dhidi ya Cape Verde, Jumanne iliyopita.

 

“Katika mchezo huo nilipata kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa Samatta, baada ya kukosa penalti aliumia sana na hapo ndipo alipoamua kujitoa kwa ajili ya kuhakikisha anafuta makosa yake hayo na kupambana ili kuiwezesha Taifa Stars kuibuka na ushindi dhidi ya Cape Verde.

 

“Alipambana vilivyo na mwisho wa siku akafanikiwa kutengeneza bao la kwanza lililofungwa na Simon (Msuva) lakini pia bao la pili alilofunga yeye mwenyewe, kwa hiyo kutokana na hali hiyo naweza kusema kuwa ameniachia ujumbe mzito ambao napaswa kuifanyia timu yangu ya Yanga kila ninapopata nafasi ya kucheza,” alisema Ajibu ambaye kwa sasa anashikilia rekodi mbalimbali katika ligi kuu msimu huu.

 

Tangu kuanza kwa ligi kuu, Ajibu ndiye mchezaji pekee anayeongoza kwa kutengeneza asisti nyingi kuliko wote akiwa na asisti 6 na amefunga mabao mawili