×

MREMBO ADAIWA KUNYWA SUMU, KISA PENZI LA MBOSSO

Mbwana Yusuf Kilungi ‘Mbosso’.

UBUYU mtamu lazima uwe mnaum-ung’unya watu wawili huku stori mbili tatu zikiendelea. Hii ni kwa sababu ubuyu wa peke yako haunogi kabisa. Ubuyu uliotufikia wiki hii unamhusu mrembo aliyejulikana kwa jina la Sherry Amour, mkazi wa Buguruni-Rozana jijini Dar ambaye anadaiwa kunywa sumu ya panya akitaka kujitoa uhai.

KISA MBOSSO

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Sherry alifanya hivyo kwa madai kuwa analizimikia penzi la mwanamuziki wa Bongo Fleva aliye chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Mbwana Yusuf Kilungi ‘Mbosso’. Ilidaiwa kuwa, kwa mujibu wa mrembo huyo, Mbosso alikuwa akimfanya ashindwe hata kula na kulala kwa kumuwaza.Chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, Sherry amekuwa akimpenda Mbosso kiasi ambacho mtaani kwao walimpachika jina la Mrs Mboso.

ATAMANI KUTAJWA KWENYE HODARI

Ilisemekana kwamba, hata katika wimbo mpya wa Mbosso wa Hodari, Sherry alitamani jamaa huyo aweke jina lake kwani alishamtumia ujumbe mwingi bila mafanikio.

“Yaani unajua sisi huku mtaani tulijua Sherry anakaribia kuchanganyikiwa na mara nyingi ukimuita Mrs Mboso alikuwa akifurahi au kuachia tabasamu na kamwe usiuponde wimbo wowote wa Mbosso.

AENDA KUNYWA SUMU

“Kuna kipindi Sherry alifunga safari hadi ofisi za WCB (Mbezi-Beach, Dar), lakini hakufanikiwa kumuona,” alisema mpashaji huyo.

Kikiendelea kumwaga ubuyu huo mchana kweupe, chanzo hicho kilisema, kuna siku walikuwa kwenye sherehe na rafiki zake, wakaanza kumtania kuwa kwa nini shemeji hakumuimba kwenye wimbo wake wa Hodari, kitendo ambacho kilimuumiza na kuamua kuondoka kwa hasira huku rafiki zake wakijua kuwa anakwenda nyumbani kulala, lakini kumbe alikwenda kununua sumu ya panya na kwenda kuinywea chumbani kwake.

“Unajua watu wengi walijua Sherry amechanganyikiwa kwa sababu alivyonunua ile sumu na kuinywa, akaanza mwenyewe kupiga kelele na kumwambia dada yake kuwa amekunywa sumu hiyo kwa ajili rafiki zake waliomzonga na kumtania kuhusu Mbosso hivyo alimpa maziwa na kumkimbiza katika Hospitali ya Mnyamani (Buguruni) ambapo alipumzishwa kabla ya kuwa sawa na kuruhusiwa,” kilisema chanzo hicho.

MSIKIE MREMBO MWENYEWE

Baada ya Ijumaa Wikienda kupata ubuyu huo lilimtafuta mrembo huyo ambapo alifunguka kuwa, jambo ambalo lilimuumiza mpaka akachukua hatua hiyo siyo Mbosso peke yake bali marafiki zake walivyokuwa

“UN­AJUA watu wengi walijua Sherry amechangan­yikiwa kwa sababu alivy­onunua ile sumu na kuinywa, akaanza mwenyewe kupiga kelele na kumwambia dada yake kuwa amekunywa sumu hiyo kwa…

wakimzonga na kumzomea ndiyo maana alikuwa kwenye hali kama hiyo.“Mimi ninajua jamii nzima haiwezi kunielewa kwa nilichofanya, lakini ile ni hasira, watu wanatakiwa wanielewe hivyo kwa sababu walikuwa kama wananizonga na kunizomea kwa nini sijaimbwa kama ni mtu wangu au najiita Mrs Mbosso, lakini sidhani kama naweza kurudia tena hivyo maana nilikiona kifo” alisema mrembo huyo.

MBOSSO SASA

Ili kupata mzani wa habari hiyo kama Mbosso anajua kuna mrembo aliyekunywa sumu kwa ajili yake, gazeti hili lilimtafuta jamaa huyo na kumpa habari hiyo ambapo alishangaa na kusema atamtafuta dada huyo maana anaonekana ana mapenzi makubwa kwake.

“Dah! Hiyo ni kali jamani, kumbe mashabiki wana mapenzi kiasi hiki. Kwa kweli nitamtafuta huyo dada, naomba tu mawasiliano yake nitamsapraizi,” alisema Mboso.

MAKALA: Imelda Mtema, DAR