The House of Favourite Newspapers

WAKATI LYNN, KIM NANA WAKIPIGANA VIKUMBO, KAKA AMCHAGULIA MONDI MKE!

WAKATI warembo Irene Charles ‘Lynn’ na Lilian Paul Kessy ‘Kim Nana’ wakitajwa kumuwania staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kaka wa mwanamuziki huyo, Rommy Jones, amefunguka kuwa mke pekee ambaye anamfaa mdogo wake huyo ni mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Ijumaa Wikienda limesheheni mahojiano.  

Rommy alifunguka hayo katika mahojiano maalum ambayo yalilenga kujua ni mrembo gani ambaye alimfaa Diamond pindi walipokuwa naye na kama kuna uwezekano akamrudia na kufunga naye ndoa.

AELEZA ANAVYOFAHAMU ZARI

Rommy aliweka wazi kuwa, Zari ni mwanamke anayejua kulea familia yake kama mama, yaani hata akiwa baba hayupo, kila kitu kitaenda sawa bila kuwa na hofu yoyote na anajua kuisimamia vyema nyumba yake kama mwanamke.

 

“Nasema ukweli ndani ya moyo wangu, Zari ni mwanamke ambaye anafaa kuwa mke na kuwekwa ndani kwa sababu anajielewa na anasimama kama mama kuanzia kwenye ulezi wa watoto wake na kila kitu ndani ya nyumba,” alisema Rommy.

 

ANGEPENDA AOLEWE ZARI

Kaka huyo alikwenda mbele zaidi na kusema kuwa kwa upande wake angependa Zari awe shemeji yake wa maisha na ikiwezekana wafunge ndoa kwani ana kila sifa ya kuwa mke na ndiye mwanamke pekee anayeweza kumuweka sawa mdogo wake na akaenda kwenye njia sahihi.

“Unajua kila familia ingependa sana kuona mtoto wao anapata kitu kilicho bora, yaani mke ambaye anaweza kusimama vyema kama mama hivyo mimi leo nikiamka Diamond aniambie anamuoa Zari, nitafurahi sana kwa sababu najua atakuwa amepata kilicho bora kabisa,” alisema Rommy.

 

AZUNGUMZIA ISHU WATOTO KUITWA KIMA

Katika mahojiano hayo, Rommy ambaye mbali na undugu ni rafiki mkubwa wa Diamond, aliweza kuizungumzia ishu ‘iliyotrendi’ hivi karibuni ya Zari kuwaita kima watoto wa msanii huyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari aliwaposti watoto wa Diamond na kusindikiza na ujumbe ulioibua utata kwa kuwaita kima.

 

Rommy alisema kitendo hicho hakikumshangaza sana kwani alichukulia kama jambo la hasira ambalo linaweza kumtokea mtu yeyote katika masuala ya uhusiano. “Ninachojua mimi kama kuna kitu kama hicho cha kuitana watoto kima, najua wazi ni hasira ya mapenzi tu, lakini hakuna kitu kingine maana mtu mkigombana mnaweza kuitana majina yote, lakini ni mambo ya kwaida tu hayo yanayotokana na hasira,” alisema Rommy.

 

AMGUSA WEMA…

Kwenye mahojiano hayo, Rommy hakusita pia kumzungumzia mrembo Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuwa na uhusiano na Diamond kisha wakamwagana.

Alisema kwa sasa mrembo huyo amebaki kuwa rafiki yao na kwamba suala la ndoa kwa Diamond kwake haoni kama lina nafasi tena. “Wema ni mshkaji sana wala haiwezi kutokea kamwe akaoana na Diamond kwa sababu kila mtu ana maisha yake ya kimapenzi na ni watu ambao wakikutana wanapiga stori kama kawaida, ameshakuwa ni rafiki yetu sana,” alisema.

VIPI KUHUSU LYNN, KIM NANA?

Akizungumzia wanawake wanaotajwa kupigana vikumbo kumrithi Zari kwa Diamond, Rommy alisema warembo hao hawezi kuwaongelea sana sababu hawana ‘mizizi’ katika himaya ya mdogo wake huyo.

“Unajua Diamond kwa hao (Lynn na Kim Nana) ni kama tu zile za mwanaume kutenda kosa na kuchepuka nje, lakini akawa na msimamo na mwanamke wake, kwa hiyo kwa hao siwezi kumuongelea sana kwa sababu pia sisi hata siku moja hatukai na kujadiliana naye mambo yake ya kimapenzi, ila ukizungumzia mke, basi nitakuambia ni Zari tu,” alisema Rommy.

 

TUJIKUMBUSHE

Diamond na Zari walidumu kwenye uhusiano kwa zaidi ya miaka mitatu na kufanikiwa kupata watoto wawili, walimwagana Februari, mwaka huu baada ya mrembo huyo kudai kuchoshwa na vitimbi vya ‘michepuko’ alivyokuwa navyo Diamond kila uchwao.

Comments are closed.