The House of Favourite Newspapers

WACHUNGAJI WAGOMBANA MO DEWJI KUPATIKANA

Nabii Daniel Shilla

SIKU chache baada ya bilionea namba moja Tanzania, Mohammed Dewji kupatikana, balaa kubwa limeibuka kwa wachungaji wawili wa jijini Dar ambapo wamejikuta wakigombana kila mmoja akisema yeye ndiye aliyetoa utabiri wa kupatikana kwake.  

Ishu hiyo ilianza Jumamosi iliyopita ikiwa ni baada ya Mo kupatikana ambapo Nabii Daniel Shilla wa Kanisa la Bethel International Ministry Tanzania akiwa anazungumza na chombo kimoja cha habari alisema yeye ndiye aliyetoa utabiri kwamba Mo atapatikana ndani ya wiki hiyo.

 

Pamoja na kukiri huko kwenye mahojiano, Shilla aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba anajivunia kuwa mtumishi pekee aliyeonyesha talanta yake. Watu mbalimbali walitoa maoni kwenye ujumbe huo ambapo mchungaji mwenzake wa Kanisa la Emmaus Bible Church Pentecostal, Daud Mashimo alimhoji kwamba huo utabiri aliutolea wapi maana hakuna mtu aliyeuona wala kuusikia.

 

WAGOMBANA

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juzi, Mchungaji Mashimo alisema baada ya kuandika maoni na kumuuliza Shilla hivyo kwenye ujumbe wake, mtumishi huyo alimwendea inbox na kumwambia anatakiwa kukaa kimya na siyo kulidhalilisha kanisa.

MESEJI ZAANIKWA

Akiendelea kufungukia kuzinguana kwao, Mashimo alianika meseji alizotumiwa na Shilla ambazo zilisomeka hivi; “Kama huna maono uwe unakaa kimya na siyo unadhalilisha kanisa, tuache wenye maono tufanye kazi ya Mungu. Sikuwahi kuhisi kama una wivu kiasi hicho nimekushangaa sana. “Nimeumia sana nimeona umekomenti na wewe ni rafiki yangu.”

 

MASHIMO AUMIZWA NA MESEJI HIZO

Mchungaji Mashimo alisema kwamba aliumizwa sana na meseji hizo ambapo baadaye mtumishi huyo alimblock kwenye Instagram. Pia Mashimo alisema kuwa, kauli ya Nabii Shilla kwamba yeye ndiye mtumishi pekee aliyetoa utabiri kwamba Mo atarudi ndani ya wiki iliyopita hakuwahi kuiona popote.

 

“Sijawahi kuona ametoa maono yoyote juu ya Mo bali mimi ndiye nilikuwa naomba na waumini wangu ili Mo arudi maana nilioneshwa na Mungu kwamba atarudi ndani ya wiki iliyopita na kweli akarudi. “Kabla ya kurudi Jumapili ya Oktoba 14, nilifanya maombi maalum kanisani kwa ajili ya Mo na nikatoa maono ambayo Mungu alinionesha kuwa atarudi akiwa salama ndani ya wiki hiyo na kweli ikawa hivyo.

Image result for MCHUNGAJI Daud Mashimo

“Ninawashangaa sana watumishi wa Mungu wanaosema uongo ili tu kujipatia sifa maana kama ni maono umeoneshwa na Mungu si unayatoa hadharani kama nilivyoyatoa mimi? Shilla hakuwahi kutoa bali amekuja kudandia tu baada ya Mo kupatikana,” alilalama Mashimo.

 

HUYU HAPA SHILLAH

Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Shillah na kumuuliza kuhusiana na kugombana na mtumishi mwenziye kisa kupatikana kwa Mo ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Mimi ndiye niliyetabiri kwamba Mo atapatikana wiki hiyo iliyopita na kweli ikawa hivyo sasa huyo Mashimo alikuja kukomenti vibaya kwenye ukurasa wangu ndiyo nikaamua kumblock. “Kuhusu hayo malumbano mimi sitaki kwa sababu inawezekana anataka umaarufu kupitia mimi, sitaki kabisa kuongelewa kwa mambo hayo.”

GWAJIMA ATAJWA

Wakati wawili hao wakigombana, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima alitajwa kuwa naye ni mmoja wa watumishi waliotoa maono yao waliyooneshwa na Mungu kwamba Mo atapatikana ndani ya wiki iliyopita lakini hakutaka kujinadi.

 

TUJIKUMBUSHE

Oktoba 11, mwaka huu mfanyabiashara MO ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba alitekwa na watu wasiojulikana na kupatikana Oktoba 20, mwaka huu baada ya kutupwa maeneo ya Viwanja vya Gymkhana jijini Dar.

Stori:GLADNESS MALLYA, RISASI MCHANGANYIKO

Comments are closed.