The House of Favourite Newspapers

DOGO JANJA , KUWA MAKINI NA SKENDO ZA MAPENZI , ZITAKUMALIZA

Dogo Janja

MIONGONI mwa mambo yaliyosumbua sana vichwa vya wapenda ubuyu Bongo, ilikuwa ni ishu ya ndoa kati ya Dogo Janja na Irene Uwoya.  Mwishoni mwa mwaka jana, picha za Dogo Janja na Uwoya wakiwa wanafunga ndoa, zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa kasi kubwa, taarifa zikaendelea kuelewa kwamba wawili hao wameoana ndoa ya Kiislam na kuwa mume na mke halali.

Habari hizo ziliibua songombingo kubwa, na kama utakumbuka, ni kipindi hichohicho cha vuguvugu hilo, ndipo mume wa zamani wa Uwoya, mcheza soka kutoka nchini Rwanda, Hamad Ndikumana alipofariki dunia kwa kile kilichoelezwa kwamba ni ugonjwa wa moyo. Wapo ambao waliamini taarifa hizo lakini wengi waliziona kama ni njia ya wawili hao kutafuta kiki. Siku zilizidi kusonga mbele na hatimaye kile kilichoonekana kama ni kiki, kikachukua sura mpya baada ya wazazi wa pande zote mbili kuanza kukizungumzia.

Wakati mwingine tukubaliane katika kutokukubaliana! Iwe ilikuwa ni ndoa au ilikuwa ni kiko, itoshe tu kueleza kwamba wawili hawa walikuwa kwenye uhusiano mzito wa kimapenzi. Kila ulipomuona Dogo Janja, pembeni yake alikuwepo Uwoya na kila alipokuwepo Uwoya, pembeni alikuwepo Dogo Janja. Baada ya takribani mwaka mmoja kupita, uhusiano wa wawili hawa ulianza kulegalega, ‘drama’ zikaanza

kuibuka na ile furaha iliyokuwepo mwanzo ikayeyuka. Uwoya akaanza kuonekana viwanja akiwa kimpango wake, na Dogo Janja naye akawa anaonekana akirandaranda mitaani akiwa na msongo wa mawazo.

Kwa mujibu wa taarifa za watu wa karibu wa wawili hao, mambo yalikuwa magumu ndani, Uwoya alikuwa akimtuhumu Dogo Janja kwamba hajatulia, anatoka na wanawake wengine tofauti tofauti, hasa wa rika lake, jambo lililoonekana kumfanya Uwoya anyooshe mikono juu. Kimsingi sarakasi zilikuwa nyingi na kwa watu waliowahi kupitia changamoto kubwa za kimaisha, watakubaliana na mimi kwamba ni mapema mno kwa Dogo Janja kuingia kwenye ‘stress’ za mapenzi, tena na mtu waliyepishana sana umri kama Uwoya.

Stress za mapenzi zinatesa mno, na kosa moja linaweza kuzalisha makosa mengine kibao. Tumesikia pia tuhuma kwamba Dogo Janja pia amewahi kuangukia dhambini na mwanadada Wema Sepetu. Marafiki wa karibu na Dogo Janja, wanaeleza kwamba tangu staa huyo wa Ngoma ya Banana amwagane na Uwoya, amekuwa ni mtu wa mawazo sana, muda mwingi anapenda kujitenga peke na hata ushahidi wa wimbo wake mpya wa Imani ni ushahidi kwamba hayupo sawa kiakili.

Kwa umri wake, Dogo Janja hatakiwi kupitia haya anayopitia lakini yeye ndiye chanzo cha yote. Ni kweli kwamba mapenzi hayana umri lakini uamuzi wa Dogo Janja kuingia kwenye uhusiano ‘serious’ na Uwoya, naweza kuufananisha na kitendo cha kupima bahari kwa ubua. Yakutokea yameshatokea, Dogo Janja umeshajifunza sasa na unachotakiwa kutambua ni kwamba utakapoendelea kulialia kwa sababu ya mapenzi, uwezekano mkubwa ni kwamba hutaweza kuinuka hapo ulipoangukia na huo unaweza mwanzo wa nyota yako kuanza kufifia.

Kiumri wewe bado ni mdogo sana, ni vizuri ukafanya mambo yanayolingana na umri wako, achana na mapenzi usiyoweza kuyamudu kiakili, kifikra na kiuchumi. Elekeza nguvu zako katika muziki kwa sababu hata hao wanaokuona kuwa wa maana, wamekujua kupitia kazi yako ya muziki. Ukishindwa kuyafanyia kazi haya, skendo za hovyohovyo za mapenzi zitakumaliza

Comments are closed.