SERIKALI kupitia Bodi ya Filamu Tanzania leo, Ijumaa, Oktoba 26, 2018 imemfungia staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu na kumtaka asijihusishe na shughuli za filamu kwa muda usiojulikana, ni baada ya picha zake chafu (za mahaba) akiwa na bwana yake raia wa Burundi kusambaa mitandaoni.
Wema aliitwa na Bodi hiyo kuhojiwa leo ikiwa ni siku moja baada ya msanii huyo kujitokeza mbele ya wanahabari na kuomba msamaha kufuatia kitendo hicho ambacho alisema anakijutia na hatorudia tena.

Wema amekuwa akijihusisha mara kwa mara na matukio ya kusambaza picha zisizo na maadili mitandaoni na amekuwa akionywa na vyombo husika lakini kipindi hiki vimeamua kumfungia kabisa kutojihusisha na mambo ya filamu.
