The House of Favourite Newspapers

BWANA MPYA WA MOBETO MAMA ATOA NENO

MAMA mzazi wa mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto, Shufaa Rutiginga ametoa neno juu ya madai ya mtoto wake huyo kupata mwanaume mpya ambaye siyo Raia wa Tanzania na kusema kuwa, yeye kama mama hana taarifa ya kuwa mtoto wake huyo ana mwanaume mwingine kama inavyoelezwa mitandaoni.

 

Katika mazungumzo yake na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita, mama huyo ambaye ilidaiwa kuwa aliwahi kumweka mwanaume huyo kwenye ‘profile’ yake na kuandika kuwa anampenda mkwe wake huyo, alikana madai hayo. Alisema siku zote huwezi kuwazuia binadamu wakiamua kusema mambo yao hivyo naye hajali maneno ya watu.

“Mimi kwa kweli sijawahi kumweka huyo mtu, lakini pia unajua kila kukicha kwenye mitandao ya kijamii kila mtu anaongea lake. “Kwa hiyo kama mtu huwaelewi, unaweza kupata tabu sana,” alisema mama Mobeto.

 

Akiendelea kuzungumza, mama huyo alisema kuwa, kwa sasa Mobeto anapiga kazi tu na hayo mambo ya kumletea wakwe hayapo na wala hana mkwe yoyote. Alisema hahitaji mkwe kwa sababu mtoto wake huyo kwa sasa ametulia na anaendelea na maisha yake mengine kabisa ya kutafuta maendeleo.

“Mambo ya mkwe yametoka wapi tena? Ninachojua sasa hivi Hamisa (Mobeto) anapiga kazi tu na si vitu vinginevyo. “Kwa sasa sihitaji mkwe wala sina maana siku akiwepo kila mtu atamjua tu, sidhani kama hiyo itakuwa ni siri,” alisema mama Hamisa.

Hivi karibuni mitandaoni kulichafuka picha za mwanaume huyo aliyedaiwa kuwa ndiye bwana mpya wa Mobeto wakati mrembo huyo akiwa ziarani nchini Marekani

STORI: Imelda Mtema, DAR

Comments are closed.