The House of Favourite Newspapers

SHOO YA WASAFI FESTIVAL, HATIMAYE DIAMOND AMPOKEA ALIKIBA WCB

LEO Jumatano, Novemba 7, 2018, mkali wa ngoma ya Mwambie Sina, Alalikiba ametoa majibu yake kuhusu mwaliko aliyopewa na CEO wa WCB, Diamond Platinumz kushiriki katika Tamasha la muziki, Wasafi Festival 2018 linalotarajiwa kuanza November 24, mwaka huu katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania na nje ya nchi.

 

Kupitia, ukurasa wake wa Instagram, King Kiba ameshukuru kupokea mwaliko huo kutoka WCB na kudai kuwa hatoshiriki kwenye Tamasha hilo kwa sasa kutokana na kuwa na ratiba zake za uzinduzi wa kinywaji chake cha MoFaya na hivyo kusema atashiriki Tamasha hilo kwa kudhamini kupitia kinywaji chake hicho cha MoFaya.

Baada ya majibu hayo ya Kiba, Diamond Platnumz baada ya kukutana na posti hiyo ya kiba aliamua kukomenti palepale kwa kumueleza kuwa uongozi wa WCB unaendelea kuwasiliana na uongozi wa RockyStar ili kuweka mambo sawa na kwamba tayari jambo hilo limeshapitishwa.

 

“Limepita hilo Ally K@sallam_sk anamcheki Seven now… #DiamondKaranga #MoFaya#WasafiFestival2018 #NewBongofleva #BongoFlevaToTheWorld🌍@WasafiFM@WasafiFestival🔥🔥🔥💰💰🔥🔥🔥 ,” ameandika Diamond.

Comments are closed.