FIRST CLASS YA AMIGO KUZINDUA ‘MAMA WA HIYARI’ – VIDEO
Kundi la First Class Modern Taarab leo Alhamisi, Novemba 8, 2018 limetangaza onesho la uzinduzi wa albamu yao iitwayo Mama wa Hiyari ambao utafanyika Ukumbi wa Hotel Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari, kiongozi wa kundi hilo Aboubakar Soud almaarufu Amigo Au Mfalme alisema uzinduzi wa albamu hiyo yenye nyimbo sita unatarajiwa kuwa wa aina yake kwa jinsi maandalizi waliyoyafanya.
Amigo amesema muziki wa Taarab kwa siku za hivi karibuni ni kama ulipoteza mwelekea tangu aliyekuwa Mfalme wa muziki huo, Mzee wa Yusuf aliyekuwa akiliongoza kundi la Jahazi kuachana nao na kumrudia muumba wake lakini yeye amepania kuurudisha kwa kasi.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL
Comments are closed.