×

IRENE PAUL: SIMUAMINI MTU KULEA MWANANGU!

Irene Paul ‘Mama Wendo

MSANII wa filamu Bongo Muvi, Irene Paul ‘Mama Wendo’, amefunguka kuwa hata siku moja haamini kumuachia mtu mtoto wake kwa sababu anataka amlee kwenye maadili yake anayopenda.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Irene ambaye anatamba katika Tamthilia ya Huba, alisema kuwa tangu amejifungua alikuwa hajaweka mdada wa kazi wa kumuangalia mtoto zaidi ya yeye kufanya kila kitu na ni kutokana na kutaka kumjua mtoto wake vizuri tangu akiwa mdogo mpaka atakapokua.

“Ukiniambia ni kazi gani nzuri ninaipenda ni kumlea mtoto wangu naona ndio kila kitu najisikia raha sana kuona hatua kwa hatua ya mtoto wangu ndio maana toka amezaliwa namhudumia mwenyewe kwa kweli siamini mtu kabisa,” alisema Irene. Mapema mwaka jana, Irene alijifungua mtoto huyo wa kike ambaye mwenye anasema anampenda kuliko chochote.