The House of Favourite Newspapers

AJALI: Naibu Waziri Nditie Anusurika Kifo – Video

Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye jana Jumapili Novemba 11, alinusurika kifo baada kupata ajali eneo la Iguguno Kata ya Mkalama mkoani Singida.

 

Naibu waziri huyo amesema alikuwa katika ziara ya kikazi lakini anamshukuru Mungu yeye na alioambatana nao katika msafara huo wametoka salama.

 

“Ni kweli tumepata ajali, ilikuwa kilomita 25 kabla ya kuingia Singida nilikuwa natokea Nzega kikazi lakini namshukuru Mungu tumetoka salama wote,” amesema.


Gari hilo lilikuwa na watu saba wakime katibu wake na dereva lakini  taarifa zinasema wote walitoka salama.

 

Comments are closed.