×

Viza yakatisha mahaba ya Zabibu, banda

BAADA ya dada Jay wa msanii wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’, Zabibu Kiba ambaye hivi karibuni alifunga ndoa na mchezaji wa mpira wa miguu, Abdi Banda kuonekana Bongo na kuzua minong’ono, mwenyewe ameibuka na kueleza kuwa viza ndiyo imekatisha mahaba yake kwa mumewe huyo nchini Afrika Kusini ambako walikuwa wakiishi pamoja tangu walipoingia kwenye ndoa.

 

Akibonga na Risasi Vibes, Zabibu alisema amekuwa akipata maswali mengi kutoka kwa watu mbalimbali kwamba imekuwaje amemwacha mumewe Afrika Kusini na kurudi Bongo ambapo alisema amerudi kwa sababu kibali cha kuishi nchini humo ‘viza’ kiliisha muda wake.

 

“Sioni kama kuna tatizo mimi kurudi mapema Bongo maana ndiyo nyumbani kwa wazazi ila sababu kubwa ni kwamba Kusini na kurudi Bongo ambapo alisema amerudi kwa sababu kibali cha kuishi nchini humo ‘viza’ kiliisha muda wake.

 

“Viza yangu ilikuwa hainiruhusu kuendelea kukaa Afrika Kusini kwa muda mrefu kwa hiyo kuna mambo nimerudi kuyaweka sawa kisha nitarudi tena kwa mume wangu kuendeleza mahaba kama kawaida,” alisema Zabibu.

Stori: MEMORISE RICHARD