MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Jacqueline Wolper, hivi karibuni alijikuta katika wakati mgumu kutokana na gauni lake kumwacha wazi sehemu ya kifuani na matiti yake kuwa wazi hali iliyomlazimu kujiweka sawa kila wakati jambo ambalo lilimnyima raha.
Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita ndani ya Klabu ya Next Door Arena, Dar ambapo Wolper alivalia gauni lililomwacha wazi sehemu kubwa ya kifua hivyo kila alipokuwa akiendelea na burudani alikuwa akikosa raha kutokana na sehemu ya matiti kutoka nje kwani kila alipoweka sawa baada ya muda hali ilijirudia ileile.
Mwanahabari alimuuliza sababu ya kubuni fasheni hiyo ya gauni iliyoonekana kumnyima raha lakini alishindwa kutoa jibu lolote na kusema ana haraka hivyo aachwe akapumzike.
Stori: Richard Bukos, Dar