The House of Favourite Newspapers

NENO ‘SHEMEJI’ lilivyotumika kuua ‘majambazi’ 7 Mwanza – VIDEO

KAMANDA wa Polisi Mkoa Mwanza, Jonathan Shanna,  amethibitisha kuuawa kwa watu saba wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, katika eneo la Kishili, Kata ya Igoma wilayani Nyamagana, mkoani Mwanza,  kwenye majibizano ya risasi na jeshi la polisi.

Shanna amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo mtaa wa Ihushi kata ya Kishili wakati jeshi la polisi likifanya doria maalum mkoani humo.

“Hilo tukio la Kishili limetokea majira ya saa 4 usiku wa kuamkia leo, na majambazi wote wameuawa wakati wa mapigano ya kurushiana risasi na jeshi la polisi na katika mapigano hayo tumekamata silaha mbili za kivita na risasi zaidi ya 71,” alisema Shanna.

Ameongeza kwamba kabla ya kutokea makabiliano ya kurushiana risasi, polisi walifanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa mmoja ambaye ndiye aliwaongoza hadi kwenye maficho yao na kuwakurupusha wengine ambao badala ya kujisalimisha walianza mashambulizi ya risasi yaliyojibiwa na polisi.
NA IDD MUMBA | MWANZA

NENO Shemeji Lilivyotumika Kuua Majambazi 7 Mwanza

Comments are closed.