The House of Favourite Newspapers

NANDY AMNASA BWANA WA WEMA

HABARI ya mjini kwa sasa ni kuhusu madai ya msanii wa kike anayefanya fresh kwenye muziki Bongo, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ kudaiwa kumnasa mwanaume anayetajwa kuwa, alikuwa akimpa jeuri ya fedha msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu.

NI MWANAUME GANI?

 

Mwanaume ambaye inadaiwa alikuwa wa Wema na sasa kajiweka kwa Nandy ni yule ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ‘bethidei pati’ ya msanii huyo iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Next Door Arena, Masaki jijini Dar alimmwagia ‘nyekundu nyekundu’ kibao katika kumtunza.

 

Kufuatia jamaa huyo kuonesha jeuri ya pesa kwa staa huyo wa Wimbo wa Ninogeshe, minong’ono ikaanza kwamba siyo bure, kutakuwa na kitu kinaendelea kati yao.

“Hawa lazima watakuwa wanajuana, kama siyo mtu wake ni bahati sana. Siyo kwa kumfanyia kufuru ile maana mimi nina muda mrefu tangu JPM kaingia madarakani sijaona pedeshee anafanya kufuru hivi,” alisikika akisema mmoja wa mashabiki waliokuwa ukumbini hapo.

 

KABLA YA SHOO HIYO

Siku chache kabla ya shoo ya Nandy yalitua madai mazito kwenye meza ya gazeti hili kuwa, Wema siku za nyuma alipokuwa kwenye uhusiano na Patrick Christopher ‘PCK’, kuna mwanaume ambaye alikuwa akimpa jeuri ya fedha lakini alikuwa hataki kujulikana.

“Nyie mlikuwa mnamjua tu PCK, siyo hivyo… kuna mwanaume mmoja wa Mwanza anaitwa Rajabu ndiye aliyekuwa akimpa Wema jeuri ya pesa, sasa alipoona zile video chafu za Wema na PCK akakasirika sana, akaamua kumtosa na sasa kahamia kwa Nandy,” alidai mtoa habari huyo na kuongeza:

“Halafu sasa, keshokutwa Nandy atakuwa na bethidei pati yake, unaambiwa mwanaume huyo kapanga kwenda kumfanyia kufuru, nyie nendeni mtaona kitakachofanyika, jamaa ana pesa chafu.” Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, mara tu baada ya mwanaume huyo kutua kwa Nandy alimpangishia nyumba Masaki jijini Dar na kumnunulia gari la kifahari aina ya BMW X 1.

 

RISASI MZIGONI

Kufuatia madai hayo mazito kutufikia, waandishi wetu walifanya jitihada za kumtafuta Nandy ili aweke ukweli wa mambo ambapo walimfungia safari hadi katika nyumba anayodaiwa kupangishiwa.

 

NI USHUANI

Kwa maelekezo ya sosi wetu wa kuaminika ambaye hapendi jina lake lifahamike, waandishi wetu walifanikiwa kufika kwenye nyumba anayoishi Nandy iliyopo ushuani na kugonga geti kabla ya mlinzi kutoa ushirikiano wa kulifungua.

 

Baada ya waandishi wetu kuingia ndani na kuiona gari anayodaiwa kununuliwa staa huyo imepaki nje, waliomba kuonana na Nandy ambaye baada ya muda mfupi alitokea na kuanza kubanwa juu ya madai ya kutoka na mwanaume aliyekuwa wa Wema.

Risasi: Hongera bwana, nasikia umenunuliwa gari na bwana wa Wema.

Nandy: Bwana wa Wema? Mbona unanishtua, sielewi unaongelea nini.

Risasi: Huelewi nini, si yule bwana aliyekumwagia mapesa kule ukumbini? Kwanza niambie, alikumwagia bei gani maana ulitisha siku ile mama.

 

Nandy: Mh! Waja wana mambo sana, kwanza niseme nashtuka wewe kuniambia mambo ya bwana wa Wema, mimi yule bwana alinipa kama milioni tano hivi nilipozihesabu na nilishangaa kwani sikuwa nikijua kuwa nitapewa pesa hizo lakini si mpenzi wangu, wala sijawahi kujua kama anatoka na Wema.

Risasi: Mbona hiyo ndio habari ya mjini kwamba wewe umemnasa huyo bwana na amekupangishia na kukununulia gari, hujui?

 

Nandy: Ni kweli nilimualika kwenye pati yangu akanipa pesa kama mlivyoona lakini sina uhusiano naye wa kimapenzi na wala gari hili hajaninunulia yeye, mimi nimejinunulia mwenyewe kwa kazi zangu tu. Kuhusu nyumba nimepangishiwa na mpenzi wangu ambaye siwezi kumtaja kwa sasa ila ni mtu maarufu tu.

Risasi: Wewe na huyo bwana (Rajabu) mlijuana vipi?

Nandy: Alinipigia simu na kuniambia kuwa anataka kufanya biashara na mimi, akaniambia atakuja Dar, huwezi kuamini alikuja Dar na ikawa ndio imefika siku ya sherehe yangu ya kuzaliwa, nikamualika kwa bahati nzuri akaja.

Risasi: Hakukueleza chochote kuwa alikuwa na uhusiano na Wema?

 

Nandy: Hapana jamani na ninasisitiza kuwa sifahamu ingawa naweza kuamini kuna ukweli kwa sababu bwana huyo yupo beneti sana na Petman ambaye yupo karibu sana na Wema.

Risasi: Ulijisikiaje alipokutunza pesa zote zile wakati hamna uhusiano wa kimapenzi?

Nandy: Kiukweli hata mimi nilishangaa lakini kwa sababu alinipa, nashukuru na nimefurahi sana kwa kweli.

 

Risasi: Sawa, je mpaka sasa una magari mangapi maana naona yapo mawili hapa na nyumba yako umepanga kwa bei gani?

Nandy: Nina magari matatu, moja halipo hapa kwa sababu ya ufinyu wa nafasi, nyumba yangu nimepanga kwa milioni moja na laki tano kwa mwezi.

 

Risasi: Vipi muziki unauonaje maana umekupa jina sana.

Nandy: Dah! Muziki umenipa jina sana lakini nafikiria kuuacha mwaka 2020 kwani ninapenda sana kufanya biashara na ninategemea huko ndio pananifaa zaidi.

Risasi: Asante sana na kila la heri.

RAJABU NAYE ASAKWA

Baada ya Nandy kufunguka hayo, mwandishi wetu aliyekuwa amepewa namba ya simu ya Rajab, aliamua kumpigia ili azungumzie madai ya kuhamia kwa Nandy baada ya kuachana na Wema lakini simu yake kila ilipopigwa haikupokelewa. Naye Wema kama kawaida yake alipopigiwa simu kwenye namba yake ya kwanza haikuwa hewani lakini nyingine iliita bila kupokelewa.

Comments are closed.