
Kwa muda wa miezi miwili iliyopita iliyopita Rapa wawili wanaounda Kundi la Migos, ‘Offset na Takeoff’ waliongolea suala la kuachia albamu zao wakiwa solo na sio kama kundi.
Novemba 20, Rapa Offset alifunguka kwenye mahojiano na Billboard mambo mawili muhimu atakayoyaongelea kwenye hiyo na kusema ni ishu ya ndoa yake na mwanamuziki Cardi B na pamoja na ajali ya gari aliyoipata.
“Nitaunganisha matukio yangu yote yaliyotokea kuanzia miezi 18 au 24 iliyopita,kama kupata ajali,watoto wangu,familia yangu, na maisha yangu kuhusu ndoa.ntaongelea tofauti iliyopo kwenye maisha yangu, chini na juu kwenye tasnia ya muziki na hisia zangu kuhusu watu waliokuwa wakinihisi mimi ntaendelea kuwa mbwa mdogo na nikawa mbwa mkubwa” alisema Offset.
Offset alimaliza kwa kusema, “Sitokwenda kudanganya na kuna nyimbo nyingi tumezifanya za namna hiyo na watu wametokea kuzipenda,kwahiyo huu ni muda wake.”
Album ya Offset inategemewa kuingia sokoni Desemba 14, mwaka huu.