
Rapa LaRon Louis James maarufu kama Jules Santana wikiendi iliyopita aliamua kufanya tukio la kushangaza baada ya kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake wa muda mrefu, Kimbella Vanderhee tena mbele ya mashabiki wake kwenye Ukumbi wa Appolo.
Santana ambaye ni rapa wa Kundi la East Coast na mwigizaji wa filamu, alitamka maneno haya mbele ya mashabiki; “Huyu mwanamke amekuwa na mimi kwa muda mrefu, amekuwa na mimi kwenye vikwazo vingi vya shida na raha, nakupenda sana baby, wewe ni Malkia Wangu na ninataka kufanya hili mbele ya kila mtu.”
Jules Santana na Kimbella wamekuwa pamoja miaka 10 na kujaliwa kupata wawoto wawili ambao ni Juelz Santana James (8) na Bella Monroe James (6).