Yanga Yaipiga JKT Tanzania 3-0, Makambo na Ngassa Kama Kawa
Global Publishers November 29, 2018
SHARE THIS:
TIMU ya Yanga imeshinda bao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania leo katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu Bara. Wafungaji wa Yanga ni Heritier Makambo dakika ya 27 kipindi cha kwanza, Mrisho Ngassa dakika ya 54 na Ibrahim Ajibu dakika ya 81 kipindi cha pili.
Ushindi wa Yanga unamfanya afikishe pointi 35 na kupanda mpaka nafasi ya kwanza nyuma ya Azam FC wenye pointi 33 na Simba akiwa katika nafasi ya tatu akiwa na pointi 27 akicheza michezo 12.
Kikosi cha Yanga kilichoanza leo dhidi ya JKT Tanzania leo katika Uwanja wa Taifa.Kikosi cha JKT Tanzania kilichoanza dhidi ya Yanga.Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo (kulia) akishangilia na Ibrahim Ajibu (katikati) baada ya kutupia bao la kwanza dakika 27 kipindi cha kwanza, Deus Kaseke akiwafuata (kushoto). Kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu (kushoto) akimtoka mchezaji wa JKT Tanzania, Madenge Ramadhan.Wachezaji wa Yanga wakisalimia kabla ya kuanza mchezo wao.