The House of Favourite Newspapers

Wema Afungukia Maisha Yake ya Sasa

STAA ‘grade one’ kutoka Kiwanda cha Bongo Muvi, Wema Sepetu amefungukia maisha yake ya sasa kuwa anapenda yawe ya siri zaidi na kama ana shida ya kuzungumza vitu ambavyo vinamsibu ni vyema amtafute mtu sahihi ambaye anamuamini kwa asilimia zote.

 

Akizungumza na Ijumaa, Wema alisema kuwa, kwa sasa amekuwa makini kwa kila kitu anachofanya ili kumuweka salama tofauti na zamani ambapo mambo yake mengi yalikuwa yakivuja hovyo.

 

“Kwa kweli sasa hivi niko makini sana na kila jambo hivyo nimepitia kipindi kigumu sana mpaka sasa hivi nimeamua kujituliza kufanya vitu vyangu kiakili,” alisema Wema ambaye hivi karibuni aliingia katika ‘msala’ baada ya kuvuja video ikimuonesha akiwa katika mahaba na mwanaume aliyedaiwa ni mchumba wake, Patrick Christopher ‘PCK’.

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.