
WAKALI wawili wanaounda Kundi la Rostam (Roma & Stamina) pamoja na mkali wa Bongo Fleva, Maua Sama wamewatega mashabiki baada ya kuazisha msemo wa Tunafunga Jumla Jumla. Katika kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii, wawili hao wamekuwa wakiposti picha zao na wakati mwingine wa tukio fulani wakiambatanisha na maneno Tunafunga Jumla Jumla, jambo ambalo mashabiki wengi wamekuwa wakishindwa kung’amua maana yake.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, Roma alisema neno hilo alianza kuliona kwa Stamina lakini anashangaa wengine wameanza kuliiga huku wengi wakiomba ufafanuzi. “Ukiniuliza maana yake sielewi ila ni misemo kama ilivyo misemo mingine. Mfano Mangi anaweza kufunga duka akasema nafunga jumla jumla, au mama n’tilie, muuza maji, karanga na wengine wengi kwa hiyo suala la biashara kuna kufunga jumla jumla,” alisema Roma.