×

WANAFUNZI VINARA WA KIDATO CHA NNE, SITA 2018 WATUNUKIWA TUZO

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Kambi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri wa Afya Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza jambo.
Sehemu ya baadhi ya washindi wa kidato cha Nne na cha Sita walipokaa.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Kambi akiwatunuku vyeti vya ushindi.
Prof. Mohamed Kambi akiendelea kuwatunuku vyeti.
Washindi wa Kitaifa wa Matokeo ya Kidato cha Nne na Sita wakiendelea kupokea vyeti.

 

 

WANAFUNZI vinara  wa Kidato cha Nne na Cha sita kwa mwaka wa 2018 waliofanya vizuri katika matokeo yao ya kuhitimu  wametunukiwa tuzo za vyeti pamoja na fedha kama ishara ya kuwatia moyo katika kuongeza bidii.

 

Utoaji wa tuzo hizo umetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Kambi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambapo ametoa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya Biolojia na Kemia katika matokeo ya kidato cha Nne na cha Sita kwa mwaka 2018.

Mmoja wa walimu wanne wa masomo hayo ya Sayansi  ambao ndiyo waliowezesha wanafunzi hao kufaulu akipokea cheti.

 

Utoaji wa tuzo hizo umefanyika leo katika viwanja vya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam.

Mwalimu wa masomo ya Sayansi  ambao ndiyo waliowezesha wanafunzi hao kufaulu akipokea cheti.

 

Akizungumza katika hafla hiyo amesema kuwa nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda na hivyo kunahitajika wataalam  wa masomo ya Kemia na Biolojia kwa ajili ya kuendesha viwanda.

 

Akifafanua zaidi Prof Kambi amewatia moyo wahitimu hao akiwaasa zaidi kujituma katika kusoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao ya  sayansi.

 

Pro Kambi ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuanzisha tunzo hizo kwani inawatia moyo wanafunzi kuendelea kuvutika katika kusoma kwa bidii masomo ya Kemia na Biolojia.

 

Kwa uapnde wake Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelis Mafumiko amesema kuwa wamekuwa wakitoa tunzo kwa wanafuzi kwa kuwapa cheti pamoja na Fedha.

 

Jumla ya wanafunzi waliopata cheti na fedha ni 24 na walimu wanne wa masomo hayo ya Sayansi  ambao ndiyo waliowezesha wanafunzi hao kufaulu.

 

Aidha amesema kuwa wataendelea kuhimiza wanafunzi katika kusoma masomo ya sayansi ambayo ili taifa liweze kupata watalaam wengi hasa katika kuelekea uchumi wa viwanda.