The House of Favourite Newspapers

YANGA YAIPIGA RUVU SHOOTING BAO 3-2 TAIFA -VIDEO

Kikosi cha Yanga kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga imejipatia mabao yake kupitia kwa Amis Tambwe, Feisal Salum na Heritier Makambo aliyefunga kwenye dakika za mwisho kabisa za mchezo.

Wapinzani wao Ruvu Shooting, walifanikiwa kupata mabao yao kupitia kwa Fully Maganga na Said Dilunga aliyefunga kwa mkwaju wa penati.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga izidi kujiweka kileleni kwa kuwa na alama 44 na kuiacha Azam yenye 40 kwenye nafasi ya pili.

 

Comments are closed.