×

Maoni Ya Meek Mill Kuhusiana Na Boyfriend Mpya Wa Nicki Minaj

 

Ex wa Nicki Minaj, rapa Meek Mill amefunguka baada ya kuulizwa na shabiki kuhusiana na mchumba mpya wa Minaj ambaye ni Kenneth Petty.

 

Kupitia mtandao wa tweeter #askmeek shabiki mmoja alimuuliza rapa huyo kuwa anayaonaje mahusiano mapya ya Nicki na boyfriend wake mpya huyo?

 

Meek alijibu kwamba hajisikii chochote ila kuna wakati alikuwa anajaribu kuingia kumtafuta Nicki instagram lakini aligundua kuwa ameblokiwa.

 

 

Lakini rapa huyo mwezi uliopita alifanyiwa mahojiano na Vulture na kukanusha kwamba huwa hachati na mtu DM na kauli hiyo ilikuja baada ya Nicki Minaj kumwimba Meek kwamba anaendeleaga kumtumia meseji Dm kwenye wimbo wa ‘Barbie Dreamz’ unaopatikana kwenye album yake ya Queen iliyotoka mwaka huu.