Kikosi cha Yanga kimeibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Tukuyu Stars katika mchezo wa Kombe la Shirikisho nchini. Yanga imepata mabao hayo kupitia kwa Amis Tambwe aliyefunga matatu huko moja likiwekwa kimiani na Mkongomani, Heritier Makambo.