×

Mwanaheri na Kitchen Party Baada ya Ndoa!

Mwanaheri Hemed

MSANII wa filamu za Kibongo, Mwanaheri Hemed ameeleza sababu ya kufanya sherehe ya ‘kitchen party’ baada ya kuolewa, iliyofanyika wikiendi iliyopita katika Hoteli ya Defrance iliyopo Sinza jijini Dar.

Akizun- gumza na gazeti la Amani, Mwanaheri alisema kuwa japokuwa aliolewa tangu mwaka jana lakini ndoa ilikuwa ya harakaharaka kuwahi mwezi wa Ramadhan na hakufanya sherehe ndio maana ameamua kufanya kipindi hiki.

“Watu wengi walikuwa wa- nashangaa kwa nini nimefanya tena sherehe hii ya kitchen party wakati nil- ishaolewa kipindi cha nyuma lakini ni kwa vile huko nyuma sikufanya kabisa, nikaona ni vyema basi nifanye ili niweze kujumuika na ma- rafiki zangu wafurahi pamoja na mimi,” alisema Mwanaheri.

Stori: Imelda Mtema