×

GLOBAL HABARI JAN 13: SAKATA la SPIKA na CAG Lafika PABAYA! – VIDEO

Suala la Spika Job Ndugai kumtaka Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa hesabu za Serikali nchini Profesa Mussa Assad ,kufika kwenye kamati ya maadili ya bunge Januari 21, limechukua taswira mpya baada ya Uongozi wa mabunge wa jumuiya ya Madola kuahidi kulishughulikia bila kuathiri uhuru wa kikatiba wa mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini.

Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari mapema leo, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, amesema kwa kutambua umuhimu wa ofisi ya mkaguzi na mthibiti Mkuu wa hesabu za serikali nchini, amefikisha suala hilo katika uongozi wa mabunge ya jumuiya ya madola ambao wameahidi kulishughulikia bila kuathiri uhuru wa kikatiba.

Aidha Zitto amebainisha kuwa kwa ushirikiano na wabunge wengine watano akiwemo Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea ,wamechukua uamuzi wa kufungua kesi ya kikatiba mahakama kuu ya Tanzania ili kupata TAFSIRI ya kinga ya mthibiti wa hesabu za serikali na mamlaka ya spika kikatiba, hivyo kulinda uhuru wa maoni.

Spika Ndugai alitoa wito wa kumtaka Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali,Prof. Mussa Assad kufika kwenye Kamati ya Maadili na Haki ya Bunge Januari 21, kufuatia kauli aliyotoa dhidi ya Bunge akiwa New York nchini Marekani kwamb bunge ni dhaifu.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club