NDOA YA NELLY KAMWELU YANUKIA
NDOA ya Miss Universe Tanzania na Miss Southern Africa International 2011, Nelly Kamwelu inanukia baada ya taratibu za awali kuanza kufanyika huku ikielezwa kuwa, anayemuoa ni mwanaume ambaye wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Nelly alisema kuwa anamshukuru Mungu ameweza kumpata mtu ambaye anampenda na anaahidi kuwa mke bora baada ya tukio hilo la heri kukamilika.
“Unajua kila jambo na wakati wake, yamesemwa mengi juu yangu lakini nashukuru Mungu siku si nyingi nitaandika historia katika maisha yangu, kwa lugha nyingine ni kwamba naolewa ‘soon’ kwani nimeshachumbiwa,” alisema Nelly.
STORI: Imelda Mtema, Ijumaa Wikienda
Comments are closed.