The House of Favourite Newspapers

Zawadi ya Simu Yaongezwa Chemsha Bongo ya Uwazi

Zawadi ya simu kali ya kijanja imeongezwa kwenye Chemsha Bongo inayoendeshwa na gazeti hili ambapo mbali na pesa taslim shilingi 100,000 kutolewa kwa wasomaji wawili, pia msomaji mmoja atajishindia simu ya mkononi.

 

Akizungumza na gazeti hili, mratibu wa chemsha Bongo hiyo, Elvan Stambuli alisema kuwa, hatua za kuongeza zawadi hiyo ya simu imekuja baada ya kubaini kuwa, kuna kila sababu ya kuwafurahisha zaidi wasomaji.

 

“Muitikio umekuwa mkubwa sana, tangu tumeanza kuitangaza chemsha bongo hii wasomaji wengi wamekuwa wakipiga simu na kuulizia jinsi ya kushiriki, maelezo yapo kwenye gazeti hili ukurasa wa pili, kila kitu kipo wazi.

 

“Awali tulitangaza kuwa, tutatoa shilingi 100,000 kwa wasomaji wawili, yaani kila mmoja shilingi 50,000 lakini tumekaa tukaona tuongeze zawadi, kwa hiyo mbali na pesa keshi, pia tutatoa simu kali ya kijanja kwa msomaji mmoja kila wiki,” alisema Stambuli na kuongeza:

 

“Ili ushinde ni rahisi, unachotakiwa kufanya ni kununua gazeti la Uwazi, unakwenda ukurasa wa pili ambapo atakutana na kuponi yenye swali rahisi sana, atajibu kisha kutuma kwenda kwenye namba iliyowekwa, baada ya hapo atakaa mkao wa kusikilizia kupigiwa simu siku ya Ijumaa kwani huenda bahati ni yako wiki hiyo.”

Kwa maelezo zaidi endelea kununu gazeti hili na magazeti mengine ya Global Publishers au piga namba 0658 798787!

Na Mwandishi Wetu

Comments are closed.