The House of Favourite Newspapers

BREAKING: CAG ASALIMU AMRI KWA SPIKA “Nitaenda kwa Ndugai” – Video

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad, amekubali kuitikia wito wa Spika wa Bunge, Job Ndugai, aliomtaka kufike mbele ya Kamati ya Bunge ya Maadili na Haki mnamo Januri 21, mwaka huu.

 

“Majibu yangu katika mahojiano yaliyozua mjadala hayakuwa na nia ya kulidhalilisha Bunge hata kidogo, maneno kama udhaifu ni lugha ya kawaida sana kwa Wakaguzi kutoa maoni ya utendaji wa mfumo wa taasisi mbalimbali.

 

“Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Bunge ni Taasisi ambazo lazima zielewane na kufanya kazi kwa karibu sana, kwa imani yangu nina mahusiano mazuri na Bunge,” amesema Prof. Assad.

VIDEO: MSIKIE CAG AKIFUNGUKA

Comments are closed.