The House of Favourite Newspapers

Wateja 100 wa NMB wajishindia shs 100,000/- kila mmoja za ‘MastaBata’

Meneja wa Benki ya NMB  Tawi la Oyster Plaza, Hildegard Mng’ong’o akizungumza  kwenye droo ya tano ya Masta Bata.
Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi Benki ya NMB, Manfredy Kayala (kulia) akizungumza.
Remida Mosi (kulia) kutoka Benki ya NMB kitengo cha Kadi akizungumza.
Remida Mosi (kulia) kutoka Benki ya NMB kitengo cha Kadi akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tano.
JUMLA ya wateja 100 wa Benki ya NMB wamejishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- kila mmoja na wengine sita wakijishindia simu janja ‘Samsung S9+’ zenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/- kila moja. Idadi ya wateja hao imefikiwa leo baada ya kuchezeshwa droo ya tano ya shindano la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya ‘NMB Mastercard’ au ‘NMB Masterpass’ linalojulikana kama ‘MastaBata’ na wateja wengine 20 kujipatia kitita hicho.
Droo ya tano imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam katika Tawi la NMB Oyster Plaza na kupatikana kwa washindi hao 20 chini ya uangalizi wa Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdallah Hemedy.
Akizungumza katika droo hiyo Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi Benki ya NMB, Manfredy Kayala Alisema wateja 20 wamepigiwa simu na kujulishwa ushindi wao na fedha walizojishindia zitaingizwa kwenye akaunti zao ndani ya saa 24 tangu kuchezeshwa kwa droo hiyo.
Alisema kupatikana kwa washindi wa leo kunatimiza idadi ya wateja 100 hadi sasa ambao wamejishindia shilingi 100,000 kila mmoja, huku kukiwa na wengine 6 walionyakuwa simu aina ya Samsung S9+’ droo iliyopita.
Alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa ‘NMB Mastercard’ au ‘NMB Masterpass’ na wao kujishindia zawadi hizo.
Hata hivyo, aliwaomba wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea na takribani wateja 200 watanufaika na shindano zima.

Comments are closed.