
REAL Madrid ipo kwenye harakati za kuhakikisha wanamnasa staa wa Tottenham Hotspur, Christian Eriksen.
Klabu hiyo imekuja na janja sasa ya kumtumia James Rodríguez ili kuwalainisha Spurs wamwachie Eriksen kirahisi.
Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy inasemekana amekuwa mgumu kumwachia kiungo huyo mshambuliaji.
Real Madrid inataka kumtumia Rodriguez katika mpango wa kutoa hela na mchezaji ili kumnasa Eriksen.
Rodriguez kwa sasa anachezea kwa mkopo katika timu ya Bayern Munich ingawa amekuwa na wakati mgumu wa kupata namba.

Tangu Bayern imekuwa chini ya kocha Niko Kovac. Rodriguez amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.
Wakati akisugua benchi, Rodriguez akapata mkosi mwingine kuumia goti na enka kwa nyakati tofauti.
Real Madrid ikifikiria kumtoa Rodriguez lakini staa huyo wa Colombia anafukuziwa pia na timu za Arsenal na Napoli.
