×

Rapa DMX Kutoka Gerezani Januari 25

 

RAPA wa Marekani, Earl Simmons, maarufu kama DMX anategemewa kuachiwa huru siku ya ijumaa January 25 baada ya kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

 

Mwanasheria wake ameliambia shirika la habari la ‘Vulture’ kwamba, “Niliongea naye, alikuwa mwenye furaha, anatazamia kuwa nyumbani kesho.”

DMX alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja Machi 2018 baada ya kupatikana na kosa la ukwepaji wa kodi.  Aliingia jela mapema januari mwaka 2018 baada ya kutohudhuria vipimo vya utumiaji wa madawa huku akisubiria adhabu yake ya kesi ya kukwepa kodi.